Uoto asilia
Uoto asilia (au Uoto wa asili) ni mimea yote inayoota kiasili, tofauti na ile inayooteshwa na binadamu. Kwa hali hiyo uoto wa asili huhusiana moja kwa moja na tabia ya nchi, kwa mfano nyasi, msitu, vichaka na mbuga.
Tundra Taiga Temperate broadleaf and mixed forest Temperate grasslands Subtropical moist forest Mediterranean Monsoon forest Jangwa Xeric shrubland Dry steppe Nusu-jangwa Grass savanna Tree savanna Tropical and subtropical dry forest Tropical rainforest Alpine tundra Montane forest
Msitu ni mkusanyiko wa miti mirefu na mikubwa ambayo huota sehemu kubwa kwa kukaribiana na vichaka ambavyo ni miti midogomidogo na mifupi iliyokusanyika kwa pamoja sana na mbuga ni uoto wa kisavana ambao ni kama nyasi.
Uoto wa asili ni matokeo ya athari za hali ya hewa, ambayo nayo huhusiana na kuathiriwa na sura ya nchi. Kwa mfano misitu minene hustawi katika sehemu za milima zenye mvua nyingi.
Aina na kiasi cha uoto wa asili hubadilika kadiri mvua inavyobadilika. WUtunzaji wa uoto wa asilia ni njia bora ya kuwezesha maisha ya afya katika jamii kwa maana kupitia njia mbalimbali za uoto wa asili kuna mvua, hewa nzuri, makazi ya wanyama. na kama utunzaji wetu wa uoto wa asilia utakuwa bora, basi utatusaidia sisi pamoja na vizazi vijavyo mbeleni.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uoto asilia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |