Basilika la Mt. Petro
Basilika la Mt. Petro mjini Roma ni kanisa kubwa kuliko yote duniani na linatumiwa sana na Papa, ingawa si Kanisa kuu la jimbo lake.
Basilika hilo lote liko ndani ya eneo la Vatikani ambalo ni dola au nchi huru ndogo iliyoko ndani ya mji wa Roma (makao makuu ya Italia).
Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[1].
Historia
haririKanisa hili lilianzishwa mnamo mwaka 324 na Kaisari Konstantino Mkuu aliyeagiza ujenzi mahali ambapo watu waliamini Mtume Petro aliuawa kwa ajili ya imani ya Ukristo akazikwa wakati wa Kaisari Nero (kabla ya mwaka 68).
Kanisa hilo la kale lilionekana bovu wakati wa karne ya 16, hivyo Papa Julius II aliamuru libomolewe ili kujenga kanisa jipya.
Muda wa ujenzi ulikuwa miaka 120: ulianza mwaka 1506 ukakamilishwa mwaka 1626.
Wasanii mashuhuri walishiriki katika ujenzi na upambaji wa kanisa hilo kama vile Raphael, Michelangelo na Gian Lorenzo Bernini.
Ujenzi wake uligharamia pesa nyingi. Wataalamu wengi huona ujenzi huu ulikuwa sababu moja ya Matengenezo ya Kiprotestanti yaani farakano na Kanisa Katoliki lililoanzia Ujerumani katika karne ya 16.
Ni kwamba Mapapa walianzisha kodi mpya kwa waumini ili waweze kuendeleza ujenzi. Madai ya pesa kwa ajili ya ujenzi huo yaliendeshwa kwa ukali uliosababisha upinzani wa Martin Luther na wengine, hasa huko Ujerumani.
Vipimo
haririKanisa hilo lililojengwa juu ya eneo la mita za mraba 15,160 linaweza kupokea umati wa watu 60.000.
Lina urefu wa mita 211.5 na kimo cha mita 132.5.
Ukumbi wake una urefu wa mita 187 na upana wa 27.50. Ukumbi wa pili una urefu wa mita 138.
Jengo lina kuba moja kubwa na makuba manane ya kando.
Ndani ya kanisa kuna altare 45, nguzo 800, sanamu kubwa 390 za watu wa Biblia, Watakatifu na Mapapa.
Picha
hariri-
Uwanja wa Mt. Petro mbele ya kanisa.
-
Sanamu ya Mtume Paulo mbele ya kanisa.
-
Sanamu nyingi zinapamba dari la kanisa.
-
Mlango huu wa "geti takatifu" hufunguliwa tu kwa nafasi maalumu.
-
Dirisha la Roho Mtakatifu lilitengenezwa na Bernini.
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- stpetersbasilica.org Largest online site for the Basilica
- Fullscreen Virtual Tour by Virtualsweden Archived 3 Julai 2008 at the Wayback Machine.
- Google Maps Satellite image of the Basilica
- St Peter’s Basilica and St Peter’s Tomb
- Circus of Nero and the old and new Basilicas superimposed, showing the tomb of Peter
- St. Peter's Basilica Photo Gallery Archived 11 Machi 2007 at the Wayback Machine. 249 photos
- St Peter's Basilica, Rome pictures and virtual reality movies
- Basilica of St Peter, Rome by Activitaly Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia Catholic Encyclopedia article
- Vatican City, Piazza San Pietro Archived 9 Mei 2007 at the Wayback Machine. VR panorama with map and compass effect by Tolomeus
- The pipe organs of St Peter's Basilica Archived 6 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- Vatican City, Piazza San Pietro Archived 15 Juni 2007 at the Wayback Machine. QTVR panorama hi-res (15 Mb) by Tolomeus
- St. Peter's Basilica Floor Plan
- The Bells of St. Peter's Basilica at Vatican
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Basilika la Mt. Petro kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |