Fransisko Solano
Fransisko Solano, O.F.M. (jina la Kihispania kwa kirefu lilikuwa: Francisco Sánchez-Solano Jiménez; Montilla, Córdoba, Andalusia, Hispania, 10 Machi 1549 - Lima, Peru, 14 Julai 1610) alikuwa mtawa wa urekebisho wa Wareformati wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki.
Ili kuokoa watu alifanya umisionari katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini, akihubiri na kutoa ushuhuda wake kwa Waindio na kwa wakoloni pia upya wa maisha ya Kikristo[1].
Papa Klementi X alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Juni 1675, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Desemba 1726.
Sala yake
haririYesu mwema, mkombozi na rafiki yangu!
Nina kitu gani usichonipa wewe? Najua nini usiyonifundisha wewe?
Nina thamani gani usipokuwa nami?...
Ndiwe uliyeniumba, tena bila ya kuniuliza. Wewe umeniumba.
Elekeza macho yako kwangu, Bwana, na unihurumie, kwa kuwa mimi ni mkiwa na maskini...
Kwa nini, Bwana Yesu wangu, wewe umesulubiwa, nami nasaidiwa na watumishi wako?
Kwa nini wewe uchi, nami nina vazi?
Kwa nini wewe umepigwa makofi na kutiwa taji la miba, nami nimepewa vitu vyema na kufarijiwa na fadhili nyingi?...
Mungu wa roho yangu, utukuzwe kwa yale uliyonijalia!
Bwana wangu, nafurahi kwamba u Mungu; jinsi hilo lilivyo zuri!
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Francis Solano Archived 4 Juni 2012 at the Wayback Machine. at Patron saints Index Archived 29 Agosti 2013 at the Wayback Machine.
- St. Francis Solano Archived 15 Agosti 2007 at the Wayback Machine. at "Saints Alive"
- (Kihispania) San Francisco Solano Archived 17 Juni 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |