Novemba
mwezi wa kuminamoja katika mwaka
Okt - Novemba - Des | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Mwezi wa Novemba ni mwezi wa kumi na moja katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na neno la Kilatini novem, maana yake ni "tisa", kwa vile katika kalenda ya kale ya Warumi, mwezi huo ulikuwa wa tisa. Mwaka wa 153 KK lakini, mwanzo wa mwaka ulitanguliza miezi miwili kutoka Machi kwenda Januari, na maana ya jina lake Novemba ilipotea.
Novemba ina siku 30, na inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Machi, na pia na Februari ila katika miaka mirefu yenye siku 366.