Nenda kwa yaliyomo

Jasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 15:23, 7 Oktoba 2021 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango) (Viungo vya Nje)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Jasi

Jasi (ing.gypsum) ni madini yanayoptikana mahali pengi ambayo kikemia ni sulfati ya kalsi . Fomula yake ni CaSO4·2H2O. Ni madini laini sana yakiwa na ugumu wa 2 kwenye skeli ya Mohs. Inaweza kukwaruzwa kwa kucha.

Kiasili inapatikana mara nyingi kama fuwele; jasi safi haina rangi lakini ikichanganywa na madini mengine kuna fuwele za rangi kadhaa. Kwa matumizi ya kibinadamu huchomwa ikipatikana baadaye kama unga nyeupe. Unga wa jasi unaweza kuchanganywa na maji ukipokea umbo lolote baada ya kukauka tena.

Jasi imetumiwa tangu kale katika ujenzi, hasa kwenye lipu. Katika ujenzi wa kisasa bao za jasi na matofali ya jasi hutumiwa kujenga kuta za ndani zisizobeba mzigo. Kuta hizi za jasi huzuia au kuchelewesha moto ndani ya nyumba[1]. Hutumiwa pia kama dawa la kilimo na chalki ya ubao shuleni. Wasanii hutumia jasi kwa sanamu.

  1. https://www.usgs.gov/centers/nmic/gypsum-statistics-and-information, tovuti ya National Minerals Information Center, Marekani

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.