Nenda kwa yaliyomo

Crawl

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 20:27, 28 Septemba 2024 na Muddyb (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Crawl
Imeongozwa na Alexandre Aja
Imetayarishwa na Craig Flores
Sam Raimi
Alexandre Aja
Imetungwa na Michael Rasmussen
Shawn Rasmussen
Nyota Kaya Scodelario
Barry Pepper
Muziki na Max Aruj<br<Steffen Thum
Sinematografi Maxime Alexandre
Imehaririwa na Elliot Greenberg
Imesambazwa na Paramount Pictures
Imetolewa tar. July 12, 2019
Ina muda wa dk. Dk. 87
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $13.5–15 milioni
Mapato yote ya filamu $91 milioni

Crawl ni jina la kutaja filamu ya kutisha na kusisimua ya mwaka wa 2019. Filamu iliongozwa na Alexandre Aja huku ikiandikwa na ndugu wawili akina Michael na Shawn Rasmussen.

Filamu inaeleze mgogoro wa maisha na mauti uliosababishwa na mafuriko makubwa na shambulizi la mamba. Hii ni filamu inayochanganya mandhari ya janga la asili na uwindaji wa mnyama hatari, ikiweka wahusika katika hali ya wasiwasi na vitisho vya mara kwa mara.

Muhtasari wa hadithi

[hariri | hariri chanzo]

Hadithi inamwelezea Haley Keller (anayechezwa na Kaya Scodelario), mwanariadha wa kuogelea, ambaye anarudi nyumbani kwake huko Florida kumsaidia baba yake, Dave Keller (anayechezwa na Barry Pepper), wakati kimbunga kikubwa kinapokaribia.

Baada ya kutomkuta baba yake, Haley anajikuta akiingia kwenye nyumba ya familia yake iliyojaa maji wakati mafuriko makubwa yanapoanza. Wakiwa wamenasa kwenye sehemu ya chini ya nyumba (basement), wanakabiliwa na tishio kubwa zaidi — kundi la mamba wakubwa na wakali wanaoingia ndani kwa sababu ya mafuriko.

Angali maji yanaendelea kupanda na hatari ya kimbunga inaongezeka, Haley na baba yake wanapambana sio tu na hali mbaya ya hewa na mafuriko, lakini pia na mamba hawa wenye njaa, wakifanya kila wawezalo ili kujiokoa.

Azimio la mwisho ni Haley kutumia kipawa chake kikubwa cha kuogelea kufikia uso wa nyumba yao. Kwa taabu, anafika. Anafanikiwa kumtoa babaye aliyebaki chini ya nyumba, akiwa katika mughma kati ya uhai na mauti, Haley anafikiwa kumvuta babaye aliyekaribia mlango wa mauti.

Wanachukuzana kwenda juu, dhoruba linakuwa kali zaidi. Vitisho vinaongezeka. Keller anatafunwa mkono mmoja na mamba ilhali Haley anaokoka katika shambulio lingine la mamba mwenye kiu ya damu.

Kwa taabu anafikia paa la nyumba. Bahati ikawa upande wake babaye alikuwa amefika tayari. Wanashikana mkono kusaidiana. Mwisho filamu inaisha helikopta ikisogea upande tayari kwa uokoaji.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]