Nenda kwa yaliyomo

Chinua Achebe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chinua Achebe

Amezaliwa 16 Novemba 1930
Ogidi, Nigeria
Amekufa 21 Machi 2013
Boston, Marekani
Nchi Nigeria
Majina mengine Albert Chinụalụmọgụ Achebe
Kazi yake Mwandishi

Chinua Achebe (jina la kuzaliwa: Albert Chinụalụmọgụ Achebe; 16 Novemba 1930 - 21 Machi 2013) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Nigeria.

Ameandika vitabu vingi vyenye riwaya, mashairi na insha. Hadithi zake zinatumia mitindo ya fasihi simulizi ya lugha yake ya asili, Kiigbo. Hata hivyo ameandika hasa kwa Kiingereza. Baadhi ya maandiko yake ni:

Kitabu chake cha Things Fall Apart, ambacho kinaaminika ndicho kitabu chake bora zaidi, ni kitabu kilichosomwa kwa wingi zaidi katika vitabu vya tamthiliya ya Kiafrika.[1]

Alilelewa na wazazi wake wa kabila la Waigbo katika mji wa Ogidi, jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria.

Achebe alikuwa mwanafunzi mahiri ambapo alipata tuzo ya kujifunza udaktari lakini akabadili mawazo na kujifunza fasihi ya Kiingereza kwenye chuo kikuu cha University College of Ibadan (sasa University of Ibadan).[2]

Alipenda kujifunza masuala ya dini mbalimbali duniani na utamaduni wa Kiafrika. Baadaye akaanza kuandika hadithi akiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu.

Baada ya kuhitimu masomo yake alifanya kazi Nigerian Broadcasting Service (NBS) na baadaye akahamia Lagos.

Kitabu cha Things Fall Apart alichokiandika mwishoni mwa miaka ya 1950 kilimpatia jina kubwa duniani. Baadaye aliandika No Longer at Ease (1960), Arrow of God (1964), A Man of the People (1966), na Anthills of the Savannah (1987).

Achebe aliandika vitabu vyake kwa Kiingereza na alitetea matumizi ya Kiingereza, "lugha ya wakoloni" kwenye tamthiliya ya Kiafrika. Mwaka 1975, hotuba yake An Image of Africa: Racism in Conrad's "Heart of Darkness" ilimkosoa mwandishi Joseph Conrad kama mbaguzi wa rangi. Pamoja na kuzua utata, ilichapishwa kwenye jarida la The Massachusetts Review

Orodha ya kazi

[hariri | hariri chanzo]

Riwaya

Hadithi fupi

Ushairi

  • Beware, Soul-Brother, and Other Poems (1971) (published in the US as Christmas in Biafra, and Other Poems, 1973) ISBN 9780385016414
  • Don't Let Him Die: An Anthology of Memorial Poems for Christopher Okigbo (editor, with Dubem Okafor) (1978) ISBN 9789781560217
  • Another Africa (with Robert Lyons) (1998) ISBN 9780385490382
  • Collected Poems – Penguin Books, 2004. ISBN 1400076587
  • Refugee Mother and Child
  • Vultures

Insha,maoni ya kisiasa

Vitabu vya watoto

  1. Franklin, Ruth. "After Empire: Chinua Achebe and the Great African Novel". The New Yorker, 26 May 2008. Retrieved 7 December 2010.
  2. Carl Brucker (1992). "Chinua Achebe 1930–". faculty.atu.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chinua Achebe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.