Iota
Mandhari
Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Herufi za kawaida | |||||||
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
Δ δ Delta | 4 | Π π Pai | 80 | ||||
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
Herufi za kihistoria1 | |||||||
Digamma | 6 | San | 90 | ||||
Stigma | 6 | Koppa | 90 | ||||
Heta | 8 | Sampi | 900 | ||||
Yot | 10 | Sho | 900 | ||||
1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
Iota (pia: yodi) ni herufi ya tisa katika Alfabeti ya Kigiriki. Umbo la iota kubwa na ndogo limeendelea vilevile katika alfabeti ya Kilatini na hivyo hutumiwa vile hadi leo katika lugha zote zinazotumia mwandiko huo kama vile Kiswahili, Kiingereza na kadhalika.
Kwa matumizi ya tarakimu inamaanisha namba 10.[1]
Matamshi yake ni sawa na "i" kwa Kiswahili.
Neno iota = yodi katika tafsiri ya Biblia
[hariri | hariri chanzo]Katika tafsiri ya Biblia ya "Union Bible" neno "yodi" hutumiwa pale ambako lugha asilia ya Kigiriki inatumia "iota" .
Math 5:18: Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie. [2]
Hapa neno iota/yodi hutumiwa kumaanisha "herufi ndogo kabisa" yaani sehemu ndogo yoyote ya Maandiko matakatifu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Iota ina maana ya kumi ingawa ni herufi ya tisa. Sababu yake ni kwamba alama ya digamma imepotea katika alfabeti lakini imebaki kama tarakimu ya "sita"
- ↑ Mathayo 5:18 kwenye intaneti