Kijiji
Kijiji maana yake kwa Kiswahili ni mji mdogo. Kadiri ya mazingira, kinaweza kuwa na wakazi mia chache hadi elfu chache.
Kwa kawaida vinapatikana mbali na miji, mashambani au porini kabisa.
Kijiji kama makazi ya wakulima
[hariri | hariri chanzo]Kiasili idadi kubwa ya wanavijiji ni wakulima na asilimia ya wakazi wanaofanya kazi tofauti ni ndogo. Kihistoria watu wengu duniani waliishi katika vijiji na kujitegemea humo.
Katika nchi zilizoendelea kilimo kimebadilika na wakulima wamekuwa wachache wanaoendelea kulima mashamba yote kwa msaada wa mashine. Hapo wakazi wengine wa kijiji wanafanya kazi nje wakisafiri kila siku hadi mahali pa ofisi, duka au kiwanda.
Siku hizi kwenye Dunia kwa jumla wanadamu wanaoishi katika miji mikubwa ni wengi kuliko wale wanaoishi bado vjijini.
Kijiji kama kitengo cha utawala
[hariri | hariri chanzo]Katika nchi nyingi kijiji ni pia ngazi ya chini ya utawala wa nchi. Kwa mfano nchini Tanzania kijiji kinajumlisha vitongoji kadhaa na pamoja a vijiji vingine inafanya kata.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Types of villages (anthropogenic biomes) Archived 14 Agosti 2009 at the Wayback Machine.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |