Kikosi Cha Mizinga
Kikosi Cha Mizinga | |
---|---|
Nembo ya Kikosi Cha Mizinga.
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Kinondoni,Dar es Salaam Tanzania |
Aina ya muziki | Hip hip Rap za kigumu Hip hop za kisiasa |
Miaka ya kazi | 1998 - |
Studio | 41 Records |
Ame/Wameshirikiana na | Imam Abbas Rado Jay Moe |
Wanachama wa sasa | |
Kara Pina Gwalu Fukuda Suma Lago Msema Kweli Bekham Chatu Rage Mau |
Kikosi Cha Mizinga ni kundi la Rap na HipHop ya Bongo linalotokea wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ni kundi linaloundwa na wasanii mahiri katika fani hii ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania. Kinara wa kundi hilo ni rapa Karama MASOUD almaarufu Mulla, Kubwa Lao, ama Kiboko ya Mabitozi. Zaidi ya muziki wa Hip Hop, kundi hilo lina familia na ukwasi mkubwa wa wasanii wa fani mbalimbali. Baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo ni Gwalu Fukuda, Suma Lago, Bekham, MsemaKweli, Bekham, Chatu Rage, na mwanadada Mau.
Kundi hilo, kama ilivyo dhima ya hip hop ambayo ni kueleza ukweli na kuchangia kwenye maendeleo ya jamii, limejihusisha na bado linajihusisha na kupambana na matatizo anwai yanayoikabili nchi ya Tanzania kama vile ufisadi, tatizo la madawa ya kulevya, na uvunjifu wa haki za binadamu. Kwa hivi sasa kundi hilo linaendesha kampeni dhidi ya utumiaji wa madawa ya kulevya kwenye sanaa na nje ya sanaa ya muziki kwa ujumla.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kikosi cha Mizinga katika MySpace
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kikosi Cha Mizinga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |