Nenda kwa yaliyomo

Madhabahu (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyota za kundinyota Madhabahu (Ara) katika sehemu yao ya angani

Madhabahu (Ara kwa Kilatini na Kiingereza) [1] ni jina la kundinyota kwenye angakusi ya Dunia yetu.

Mahali pake

Madhabahu lipo jirani na kundinyota la Nge (pia Akarabu, lat. Scorpius) na Pembetatu ya Kusini (Triangulum Australe). Njia Nyeupe inapita katika sehemu ya Madhabahu.

Jina

Madhabahu ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Lipo pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia. Jina linatoka katika mitholojia ya Ugiriki ya Kale[2] ambako Zeus alitoa kiapo cha kupambana na majitu wa Titani mbele ya madhabahu au altare ya kuchomea sadaka.[3]

Nyota

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Arae yenye mwangaza unaoonekana wa 2.93 mag ikiwa umbali kutoka Dunia wa miakanuru 270 na Beta Arae yenye mwangaza wa 2.85. Kuna nyota 7 zenye sayari. Mu Arae inayofanana na Jua ina sayari nne na Gliese 676 ambayo ni nyota kibete nyekundu ina sayari nne pia.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Ara" katika lugha ya Kilatini ni "Arae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Arae, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Allen, Star names and their meanings, uk. 62

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 336 ff (online kwenye archive.org)
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madhabahu (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.