Papa mteule Stefano
Mandhari
Papa mteule Stefano aliteuliwa kuwa Papa tarehe 23 Machi 752. Kwa vile akafariki siku ya tatu, tarehe 26 Machi kabla ya kuwekwa wakfu, hakuhesabiwa katika orodha ya Mapapa tangu mwaka wa 1961. Katika hati fulani za kabla ya mwaka huo, alikuwa hutajwa kama Stefano II (na mapapa wenye jina la Stefano kuongezewa namba moja zaidi) kwa sababu katikati Kanisa liliwahi kumhesabu mtu kuwa Papa mara baada ya kuchaguliwa na kukubali, bila kusubiri apewe daraja ya uaskofu.
Kabla hajateuliwa kuwa Papa, alikuwa padre mjini mwa Roma.
Alimfuata Papa Zakaria akafuatwa na Papa Stefano II.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa mteule Stefano kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |