Texas
Texas | |||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Austin | ||
Eneo | |||
- Jumla | 695,621 km² | ||
- Kavu | 678,051 km² | ||
- Maji | 17,570 km² | ||
Tovuti: http://www.texasonline.gov/ |
Texas ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Idadi ya wakazi wa jimbo lote hufikia watu 24,326,974 (2008) wanaokalia eneo la 696,241 km² ambalo ni hasa milima na jangwa. Upande wa mashariki ni maji ya ghuba ya Meksiko. Mji mkuu wa jimbo ni Austin na mji mukubwa jimboni ni Houston. Imepakana na Oklahoma, Arkansas, Louisiana, New Mexico (Meksiko Mpya) na nchi ya Meksiko (Chihuahua, Coahuila, Nuevo León na Tamaulipas).
Historia
[hariri | hariri chanzo]Koloni ya Hispania
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kufika ya Wahispania maeneo ya Texas yalikaliwa na makabila mbalimbali ya Waindio. Tangu uvamizi wa Mexiko wa Waazteki kulikuwa na misafara kadhaa ya Wahispania kwenye pwani la Texas lakini hawakukaa. Baada ya Ufaransa kuanzisha koloni ya Lousiana katika eneo la New Orleans Hispania iliogopa uenezaji wa Wafaransa wakapeleka mapadre Mexiko waliojenga misioni kadhaa huko na mwaka 1718 mji wa San Antonio ilianzishwa. Lakini idadi ya walowezi Wahispania ilikuwa ndogo kutokana na upinzani mkali wa Waindio wenyeji.
Jimbo la Mexiko na uhuru
[hariri | hariri chanzo]Baada ya uhuru wa Mexiko kutoka Hispania mwaka 1821 Texas ilikuwa jimbo la nchi mpya ya Mexiko. Ilhali serikali ya Mexiko ilikosa uwezo wa kuwashinda Waindio ilikaribisha walowezi kutoka maeneo ya Marekani kuja Texas. Kuingia kwa walowezi wengi wenye lugha na utamaduni wa Kiingereza kutoka Marekani kulisababisha kutokea kwa tofauti ya kiutamaduni na na sehemu ya wakazi wapya hawakukubali mamlaka ya serikali ya Mexiko. Hatimaye mwaka 1836 walowezi Wamarekani katika jimbo walitangaza Jamhuri ya Texas kuwa nchi huru ya kujitegemea ilivumiliwa na Mexiko baada ya vita fupi lakini Mexiko iliendelea kudai mamlaka juu yake.
Utekaji na Marekani
[hariri | hariri chanzo]Nchi hii mpya ilikuwa dhaifu na wakazi wengi waliogopa kuvamiwa upya na Mexiko. Kwa hiyo viongozi waliomba kuingizwa katika Marekani. Ilhali Texas ilikuwa na sheria ya utumwa na ndani ya Marekani majimbo ya kukubali na kukataa utumwa yalivutana kwa miaka kadhaa hapakuwa na azimio kuhusu ombi la Texas. Maana majimbo yaliyopinga utumwa hayakutaka kuongeza maeneo penye utumwa ndani ya Marekani. Lakini mwaka 1846 raisi mpya James K. Polk alitangaza utekaji wa Texas na Marekani na Texas ilikuwa jimbo la 28 katika Maungano ya Madola ya Amerika. Hatua hii ilisababisha vita ya Marekani na Mexiko iliyokweisha baada ya miaka miwili kwa ushindi wa Marekani mwaka 1848.
Sasa walowezi wapya walihamia Texas. Mashamba makubwa yalianzishwa yaliyolimwa na watumwa weusi walioongezeka hadi theluthi moja ya wakazi wote walikuwa watumwa mnamo 1860.
Jimbo la Marekani
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1861 Texas iliamua kujiunga na watetezi wa utumwa katika Shirikisho la Madola ya Amerika (yaani madola ya kusini au Confederated States) waliojitenga na Maungano (USA). Jimbo hili ilikuwa mbali na maeneo ya mapigano na watumwa wake walitangazwa kuwa watu huru mwishoni wa vita mwaka 1865. Katika miaka ya kwanza watu weusi waliweza kupiga kura na kushiriki katika siasa lakini polepole walinyimwa haki hizi. Chama kipya cha Democrats kilipinga nafasi ya wale waliokuwa watumwa katika siasa. Kwa njia ya matishio, kutumia mabavu na hata mauaji weusi wengi walizuiliwa kupiga kura. Baadaye bunge la Texas lililokuwa na Mademocrats wengi yaani watetezi wa utaratibu wa kale liliamua sheria zilizozuia watu weusi pamoja na raia wenye lugha ya Kihispania kupiga kura tena. Kwa mfano kila raia alitakiwa kulipa kodi fulani wakati wa kupiga kura - hii ilizuia watu maskini waipige kura na weusi pamoja na Wasemaji wengi wa Kihispania walikuwa masikini[1].
Hali hii ilibadilika tu tangu miaka ya 1960 ambako harakati ya haki za wananchi raia (ing. "Civil Rights Movement") iliyongozwa na Martin Luther King ilifaulu kuhamasisha serikali ya Washington chini ya maraisi John F. Kennedy na Lyndon B. Johnson kuanzisha sheria mpya zilizokataa ubaguzi wa rangi katika majimbo ya kusini. Ilhali sheria hizi ziliamuliwa kitaifa hasa na chama cha Democrats watu wengi wa Texas waliondoka katika chama hiki na kuhamia polepole chama cha Republican ambayo tangu miaka ya 1990 ilikuwa chama cha kwanza cha Texas.
Kiuchumi Texas imefaidika sana na kupatikana kwa mafuta ya petroli katika ardhi yake iliyokuwa msingi kwa uchumi mwenye nguvu.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]
Majimbo ya Marekani |
---|
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Texas kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Historical Barriers to Voting (archive University of Texas)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-02. Iliwekwa mnamo 2008-04-02.