Ukingo wa Magharibi wa Yordani
Ukingo wa Magharibi wa Yordani ni sehemu ya Palestina ya kihistoria kati ya dola la Israeli upande wa magharibi na mto Yordani upande wa mashariki. Eneo lake ni 5,800 km2.
Tangu vita ya 1967 kati ya Waisraeli na Waarabu iko chini ya usimamizi wa Israeli kwa jumla lakini utawala wa ndani wa sehemu kubwa iko mkononi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina. Eneo lingine la MamlakA hiyo ni Ukanda wa Gaza. Israeli imeanzisha vijiji vingi kwa walowezi Waisraeli ndani ya Ukingo wa Magharibi.
Hadi 1967 eneo hili lilikuwa sehemu ya ufalme wa Yordani ikiitwa "Yordani ya Magharibi".
Hali ya Yerusalemu ya Mashariki inayokaliwa na Waarabu hasa si wazi; Wapalestina wanaona mji huo kama sehemu ya eneo lao lakini Israeli imeingiza Yerusalemu yote chini ya mamlaka yake kama sehemu kamili ya taifa lao.
Miji muhimu nje ya Yerusalemu ni pamoja na Hebron, Nablus, Rafah, Tulkarm, Jenin, Bethlehemu na Ramallah.
Majadiliano yanaendelea kati ya Israeli, Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina na jumuiya ya kimataifa kuhusu maendeleo ya eneo hili.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ukingo wa Magharibi wa Yordani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |