Nenda kwa yaliyomo

Ununheksi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Ununheksi (ununhexium)
Jina la Elementi Ununheksi (ununhexium)
Alama Uuh
Namba atomia 116
Mfululizo safu huaminiwa kuwa metali
Uzani atomia 289 - 302 g/cm³ (kadirio)
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 18, 6
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0% (elementi sintetiki)
Hali maada mango
Mengineyo Ununheksi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara mbili tu

Ununhexi ni elementi sintetiki yenye namba atomia 116 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 289 - 302. Alama yake ni Uuh. Si rahisi kutaja tabia zalke kwa sababu imetengenezwa mara mbili tu katika maabara kama atomi moja-moja.

Jina latokana na maneno ya kilatini kwa "1" (unum) na kigiriki kwa "6" (heksa). Un-un-heksi yamaanisha hivyo moja-moja-sita yaani namba atomia ya elementi. Ununheksi ni jina la muda inawezekana ya kwamba jina lingine litatolewa kama wataaalamu hukubaliana.

Ufumbuzi

[hariri | hariri chanzo]

Elementi iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara mbili katika maabara ya taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Dubna (Urusi) kwa kuunganisha kiini atomia kimoja cha Kalsi na kiini kimoja cha Curi.

Nusumaisha yake ni fupi sana: haikudumu hata milisekunde.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Kama elementi zote za sintetiki haina matumizi bado zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ununheksi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.